ELIA MWALINGO NOW
Alhamisi, 1 Septemba 2016
OBAMA APINGA MAPINDUZI YA KIJESHI SYRIA
Obama apinga mapinduzi ya kijeshi Syria
Rais Barack Obama amesema kuwa, itakuwa ni makosa makubwa kwa mataifa ya Magharibi kutuma majeshi yake hadi nchini Syria ili kumuondoa madarakani rais wa Syria Bashar al-Assad.
Akizungumza na BBC, Obama amesema itakuwa ni makosa makubwa kuwatuma wanajeshi wa nchi kavu nchini Syria kumpindua rais Assad kwa sababu hilo pekee halitasuluhusiha matatizo ya Syria.
Rais huyo wa Marekani amerejelea maoni yake ya awali kuwa haina maana kwa makundi ya waasi kama vile Islamic State ndani ya Syria, kuendelea na makabiliano huku akisema kuwa jeshi la taifa hilo pekee lafaa kukomesha mapigano nchini humo.
Ameongeza kusema hii itakuwa vigumu mno huku akiongeza kusema kuwa ni muhimu kuendelea kushambulia ngome za Islamic State ndani ya Syria kwa pamoja na kuzidisha juhudi za kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya muda mrefu nchini humo.
Katika mahojiano ya kina, Bw Obama amesisitiza hitaji lake kuwa matatizo ya kimataifa inahitaji uwajibikaji wa muda baada ya muda.
Obama anasema kuwa itakuwa vigumu kwa majeshi yake ama hata muungano unaongozwa na Marekani kuitokomeza kabisa Islamic State katika kipindi cha miezi 9 za uongozi wake.
Cha mno anasema ni kudidimiza maeneo inayokalia IS na kushambulia ngome zake.
Aidha Obama anasema mashambulizi yatalenga haswa kukatiza msururu wa wapiganaji wanaoenda ulaya na kusababisha maafa makubwa.

WAKESHA KUSUBIRI KUPATWA KWA JUA
Wakesha kusubiri kupatwa kwa jua
Mbarali. Umati wa watu umepiga kambi eneo la Rujewa, wakisubiri tukio la kupatwa kwa jua kipete linalotokea baadaye leo.
Katika eneo hili ambalo awali halikuonekana kuwavutia wapita njia hata kufaa kutumika kama sehemu ya kujiburudisha kutokana na shughuli ya uchimbaji mawe na upasuaji kokoto, usiku huu watu wamejaa huku watu wakijiburudisha.
Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia watu wakiingia na kutoka eneo hilo, ambalo wataalam wa anga wameweka mitambo yao kwa ajili ya kuratibu tukio hilo la kihistoria.
Mama lishe, wachoma nyama na wauzaji wa vinywaji vikali wapo kazini kuwahudumia watu waliofika kushuhudia tukio hilo.
“Kwa kweli tukio hili ni kukumbukwa, muda kama huu ninakuwa nyumbani lakini hawa watu lazima wahudumiwe,” mamalishe Christina Mgaya.
Hata hivyo, uhaba wa nyumba za kulala wageni katika mji mdogo wa Rujewa umesababisha baadhi ya wageni kukosa sehemu ya kulala na kukesha eneo hilo.

Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)